LEO KATIKA IBADA JUMAPILI TAREHE 03 JUL 2016
SOMO - IMANI
MWL: CHUNGAJI AMOSI LUKANULA
MCHUNGAJI KIONGOZI KANISA LA PAG CHUKWANI ZANZIBAR AKIFUNGUA IBADA KWA MAOMBI YA NGUVU |
K | ||
Praise and Worship Team YA PAG Chukwani wakiimba wimbo wa kuabudu mwanzo wa ibada |
SOMO : IMANI
Luka 17 : 5 -6
Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani.
6 Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.
Imani maana yake ni
kutegemea au kusadiki au kutumainia au kutazamia jambo ambalo bado haujaliona. Hivyo kwa imani japo hatujamuona Mungu lakini tunasema MUNGU yupo kwa sababu tu tumesikia na kwa mioyo yetu tukaamini
Imani imegawanyika katika makundi matatu ambayo ni
1. Imani ya MUNGU ( Kiroho)
2. Imani ya Madhehebu
3. Imani ya asili ( Kibinadamu)
Chanzo cha Imani ni kusikia
Warumi 10:17 ( Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo)
Chanzo cha imani yeyote ni kusikia haijalishi ni imani ya namna gani , iwe ni imani ya kweli ama ya uongo chanzo chake ni kusikia aidha Neno la kweli ama neno la uongo kutoka kwenye chanzo cha ukweli ama uongo. Hivyo maisha yetu yanaathiriwa na yale tunayo yasikia kutoka vyanzo mbalimbali
Kwa leo tuishie hapa jumapili ijayo MUNGU akipenda tutaendelea na somo letu hili juu ya Imani tutaanza kuichambua imani ya Kimungu . Barikiwa
BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO KATIKA IBADA YA LEO
0 comments:
Post a Comment