Sunday, May 1, 2016

IMANI YA UZIMA IPO MOJA TU, ISHINDANIE.


( Waebrania 12:2, tukimtazama YESU, mwenye
kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu;
ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele
yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu,
naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi
cha MUNGU.)
Leo nazungumzia kuishindania Imani ya uzima
ambayo ipo moja tu.
-Imani Ya Uzima Hushindaniwa.
- Imani Ya Uzima Ipo Moja Tu Yaani Wokovu
Wa YESU KRISTO, Biblia inasema

Matendo 4:12 ''Wala hakuna wokovu katika
mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina
jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu
litupasalo sisi kuokolewa kwalo.''

-Ni jina la YESU KRISTO pekee, hiyo ndio imani
ya pekee ya uzima, na imani hii ya uzima
lazima tuishindanie.
Imani hiyo ya uzima ni moja tu na chanzo
chake ni kulisikia neno la KRISTO na kumpokea
kama BWANA na MWOKOZI wako na baada ya
hapo unatakiwa ujiunge na wana kanisa
wengine katika kuukulia wokovu na kuomba.

''Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na
kusikia huja kwa neno la KRISTO.-Warumi
10:17''

-Hiyo ndio imani ya kweli ambayo unaipokea
baada ya kulisikia Neno la KRISTO YESU na sio
vinginevyo.
Ndugu, shika yote yanayoelekezwa katika Imani
ya KRISTO kupitia Biblia maana yaliyo nje na
KRISTO ni dhambi.

''Na kila tendo lisilotoka katika imani ni
dhambi.Warumi 14:23b''

Imani Haishindaniwi Kwa Mapigano Bali Kwa
Matendo Mema Ya Kumpendeza MUNGU tukiwa
ndani ya imani hii ya uzima.
Hatutakiwi kuitwa tu wakristo bali tunatakiwa
kuitwa wakristo walio na KRISTO ndani yao. Ni
imani ya ndani kabisa ya moyo wa mtu, ni
uhusiano wa ndani kabisa kati ya mwanadamu
na muumba wake.
Ukiipokea imani hii ya uzima , Biblia inasema
hivi

''Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO
amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita
tazama! Yamekuwa mapya.-2 Kor 5:17''

Kwanini Tunatakiwa Tuishindanie Imani Ya
KRISTO?
= Ni Kwa Sababu Ndio Imani Pekee moja tu Ya
Uzima Wa Milele

Yuda 1:3 ''Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii
sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni
wetu sisi sote, naliona imenilazimu
kuwaandikia, ili niwaonye kwamba
mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu
mara moja tu. ''

=Ni kwa sababu kuna wakati mwingine kuna
kupita kwenye nyakati ngumu na kupingwa.

Wafilipi 1:27-29 '' Lakini mwenendo wenu na
uwe kama inavyoipasa Injili ya KRISTO, ili,
nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo,
niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara
katika roho moja, kwa moyo mmoja
mkiishindania imani ya Injili; wala hamwaogopi
adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni
ishara mathubuti ya kupotea, bali kwenu ninyi
ni ishara ya wokovu, huo utokao kwa MUNGU.
Maana mmepewa kwa ajili ya KRISTO, si
kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; ''

-Katika Imani Yetu Ya Uzima Tunatakiwa
Kujitahidi Sana Katika Yale Yanayompendeza
MUNGU.

2 Petro 1:5-11 ''Naam, na kwa sababu iyo hiyo
mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani
yenu tieni na wema, na katika wema wenu
maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika
kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu
utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa
ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.
Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa
tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si
watu wasio na matunda, kwa kumjua BWANA
wetu YESU KRISTO. Maana yeye asiyekuwa na
hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali,
amesahau kule kutakaswa dhambi zake za
zamani. Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi
kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu;
maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.
Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia
katika ufalme wa milele wa BWANA wetu,
Mwokozi wetu YESU KRISTO.''.

-Tunaposema Tunaishindania Imani Maana
Yake Tunafanya Yale Tu Yanayokubalika Na
Imani Hiyo Ya Uzima.
-Kwenye Imani Ya Uzima Lazima Tujue
Kwamba Tunashindana Na Maadui Ambao
Wanataka Kututoa Kwenye Imani Hiyo Pekee Ya
Uzima
Maadui Hao Ni
-Shetani Na Majeshi Yake,
-Dunia Na Anasa Zake
-Pamoja Na Mwili Na Matakwa Yake.
Hivyo Tukijua Tuko Kwenye Mashindano Na
Tuvumilie Maana Tumepewa Imani Sio Kuamini
Tu, Bali Na Kuishindania Na Kuteswa Pia Kwa
Ajili Ya Imani

Wafilipi 1:29 ''Maana mmepewa kwa ajili ya
KRISTO, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa
ajili yake;.''

-Katika Imani Lazima Tuzae Matunda Na
Kumpendeza MUNGU.

Wakolosai 1:10 ''mwenende kama ulivyo wajibu
wenu kwa BWANA, mkimpendeza kabisa;
mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi
katika maarifa ya MUNGU; ''.

-Katika Imani Lazima Kusaidiana Kiroho.
Wafilipi 4:3-6 '' Naam, nataka na wewe pia,
mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa
maana waliishindania Injili pamoja nami, na
Klementi naye, na wale wengine waliotenda
kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo
katika kitabu cha uzima. Furahini katika
BWANA sikuzote; tena nasema, Furahini. Upole
wenu na ujulikane na watu wote. BWANA yu
karibu. Msijisumbue kwa neno lo lote; bali
katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja
na kushukuru, haja zenu na zijulikane na
MUNGU. ''

Shika Imani Ya Uzima Daima siku zote wala
usisitesite.

MUNGU anasema.
''Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani;
Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha
naye.- Waebrania 10:38''

MUNGU aliye hai akubariki.
By Peter M Mabula.

0 comments:

Post a Comment