Sunday, May 1, 2016

TUMTAFUTE MUNGU MAADAMU ANAPATIKANA.

kanisa Zanzibar


BWANA YESU atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze.
Mithali 8:17 ''Nawapenda Wale Wanipendao, Na Wale Wanaonitafuta Kwa Bidii Wataniona.''.
-Maombi ni njia ya mawasiliano kati ya MUNGU na watoto wake waliosafishwa kwa damu ya mwanawe wa pekee YESU KRISTO. -Maombi ndio mawasiliano kati yetu wanadamu na MUNGU Baba yetu. Ili uhusiano wetu na MUNGU uwe hai lazima tuwe waombaji. Zaburi 62:8.'' Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; MUNGU ndiye kimbilio letu. ''
-MUNGU huongea na sisi kwa njia ya neno lake kupitia kusoma kwetu Biblia na huongea na sisi kupitia watumishi wake, na sisi tunaongea na MUNGU kwa njia ya maombi, hivyo ili uhusiano wetu na MUNGU uwepo lazima tuwe na muda wa maombi.
-BWANA Anatutaka Tumtafute Kwa Maombi
- Tumtafute Kwa Matoleo
-Tumtafute Kwa Matendo Mema
-Tumtafute MUNGU Kwa Kumtegemea Yeye Peke Yake.
-Tuombe Kwa Jina La YESU KRISTO Pekee(Yohana 14:13-14, Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. )
-Kila mtu ana wajibu wa kumtafuta MUNGU kwa maombi
- Maombi ni maisha ya waenda mbinguni.
-Maombi ni mkono mrefu wa kupokea baraka kutoka kwa MUNGU.Maombolezo 3:25 "BWANA Ni Mwema Kwa Hao Wamngojeao, Kwa Hiyo Nafsi Imtafutayo.".
-Ndugu mtafute BWANA.
MAOMBI NI MAISHA YA WATEULE, NA ILI UFANYE VYEMA NI MUHIMU KUJUA HAYA.
1. Tumtafute MUNGU Hata Hivyo MUNGU Hawi Mbali Na Kila Mmoja(Matendo 17:26-27, Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; ili wamtafute MUNGU, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.).
2. Tumtafute MUNGU Kwa Imani(Waebrania 11:6, Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. ).
3. Tuombe, Tumtafute Na Tubishe Kwenye Ufalme Wake ili tupokee baraka (Mathayo 7:7, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; ).
4. Mjue Kwanza MUNGU kwa kumcha na ukizingatia kumcha MUNGU hakika utakuwa unamjua. (Mithali 2:4-5, Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua MUNGU.).
5. Omba bila kukoma na uzimzimishe ROHO MTAKATIFU.(1 Thesalonike 5:17-19 ,ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya MUNGU kwenu katika KRISTO YESU. Msimzimishe ROHO;)
MUNGU Ameahidi Kwamba Tutamuona Kama Tu Tukimtafuta Kwa Bidii(Yeremia 29:13, Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. ).
Tumtafute BWANA Wa Mabwana Maadamu Anapatikana, Tumwite Maadamu Ya Karibu Ila Mtu Mbaya Aache Dhambi Na Arejee Kwa BWANA Naye Atamrehemu(Isaya 55:6-7, Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa. ).
BWANA YESU Anatupenda Sana.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

0 comments:

Post a Comment