Monday, July 4, 2016

UFALME WA MUNGU


MCHUNGAJI KIONGOZI KANISA LA PAG CHUKWANI MCH AMOSI LUKANULA AKITOA MAELEKEZO YA IBADA




UFALME WA MUNGU
Mathayo 3:1-2
              Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. 

Mathayo 4:17
              Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. 

M/KITI WA VIJANA BARAKA MHUNDA AKIFUNDISHA


Maana ya ufalme wa Mungu 
                Ufalme wa MUNGU ni utawala wa Mungu Mbinguni ulio katika mfumo wa Kifalme. Pia una weza ukauita Ufalme wa Mbinguni. 

                 Pia Mbinguni  ni makao makuu ya mungu ambaye ndiye Mfalame na ni nchi iliyo bora
Isaya 66:1   Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani? 

Ebrania 11:13-16   (13 Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.
14 Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe.  15 Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea.
16 Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji. )


                     Sasa ilikuwaje Yohana akaanza kuhubiri kwamba watu watubu kwa maana ufalme wa Mbinguni umekaribia na hata YESU mwanzo wa injili yake alianza pia kuhubiri habari za Ufalme wa MUNGU kuwa umekaribia?

                      Kusudi la Mungu kumuumba mwanadam ilikuwa ni kupanua ufalme wake uliopo Mbinguni uwe na duniani na akampa mwanadamu mamlaka  na ufalme wa kutawala vyote vilivyokuwa duniani
         
Mwanzo 1:26     Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 

                         Tunaona hapa Mungu anamfanya mtu kwa mfano wake yani kama yeye alivyo mfalme basi pia na mwanadamu atakaye muumba naye awe mfalame wa kutawala katika dunia lakini kwa kufuata mapenzi ya mungu 

Zaburi 8:4-9  (4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?  
5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;  
6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
7 Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni;
8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.
9 Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!)


                      Hapa Bibilia inaposema umemtawaza juu ya kazi za mikono yako inamaana amemwapisha na kumpa mamlaka ya kutawala yaani kama ambavyo katika siasa baada ya uchaguzi tuliona Mheshiwa Raisi anaapishwa au anatawazwa inamaana amepewa mamlaka juu 
ya Tanzania yote,
         
Luka 17:20-21   (20 Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza;
21 wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.)

                      Kumbe Mungu alimpa mwanadamu huo ufalme wa Mungu kama maandiko yanavyo sema hapa na hili ndilo kusudi la Mungu kwa ki8la mwanadamu awe na huuo ufalme yaani atawale na kumiliki juu ya kazi ya mikono yake.
            

MWENYEKITI CA,S  AKIFUNDISHA HABARI ZA UFALME WA MUNGU


                      Sasa kama YESU anasema Ufalme  wa MUNGU upo ndani yetu na pia tumeona Mungu amemtawaza mwanadamu juuu ya kazi yote ya mikono yake inakuwaje Yohana aseme tubuni kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia pia hata yesu mwenyewe alipoanza kuhubiri alianza kwa kusema tubuni kwa maana ufalme wa mbunguni umekaribia?
      
                      Dhambi iliharibu mfumo wa utawala wa Mungu ndani ya mwanadamu na Duniani kwa ujumla
Mwanzo 3:17-19, 24  (17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;
18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi. )


24 Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.

  Kutoka 32:7-10 (Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao,
8 wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu  10  basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.



                      Baada ya mwanadamu kumwasi kwa kutenda kinyume na maagizo yake Mungu akamfukuza mwanadamu katika ile milki yake ya kifalme  kwani kwa kumsikiliza shetani na kukubali ushauli wake nakutenda maagizo yake kukasababisha nafsi ya mwanadamu ikachafuka, baada ya kufukuzwa hapo ndo kikawa chanzo cha mateso na shida kwa mwanadamu.

WAUMINI WA KANISA LA PAG CHUKWANI WAKIFUATILIA KWA MAKINI NENO LA MUNGU


                    Ule ufalme na mamlaka ambayo Mungu aliompa mwanadamu shetani akauchukua 
Luka 4:6  ( Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7   Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. )

                    Shetani anamwambia Yesu  amsujudie ili ampe vyote yani fahari ya ulimwengu kwani vyote vipo mikononi mwake lakini Yesu hakubabaika kwani huko Mbinguni aliacha zaidi ya haya ya duniani akamkemea.  

                     Sasa hii ndio sababu ya Yohana na  na Yesu pia kuhuburi habari za ufalme wa Mungu ambao shetani alikuwa ameuteka na hata manabii wengi wakatabiri habari za mfalme wa ajaabu yaani ambaye atakuja kupambana na kuukomboa ufalme ulioibiwa.

                     YESU alikuja ili kuurudisha Ufalme wa Mungu kwa mataifa yote ambao mwanadamu aliupoteza 
Luka 4:43  ( Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa. )

                      YESU akasema jambo la kwanza kwa mwanadamu ni Ufalme wa Mungu hivyo hata katika maisha yetu ya siku hizi tulizo nazo tunahitaji sana Ufalme wa Mungu kwani tukiwa nao hatuhitaji tena kuishi kawa watumwa kwani tutatawala sawsawa na neno la MUNGU.

Mathayo 6 : 31-34 ( 31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.)


NENO LA MUNGU LIKIFUATILIWA KWA MAKINI

                   Katika Ufalme wa Mungu  mtu  anaingia kwa kutubu yaani kuzaliwa mara ya pili. 
Yohana 3:1-7  ( 1 Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. 3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.  ) 


                Maana ya kuzaliwa mara ya pili ili kuingia katika ufalme wa Mungu ni kwamba Ufalme huwa unarithiwa katika ukoo mmoja hivyo katika ukoo wa kifalme ndio kutatoka mfalme  kwa hiyo na sisi ili tuurithi Ufalme wa Mungu lazima tuwe katika ukoo wa kifalme ndio maana kwa kumwamini Yesu anatufanya watoto wa Mungu.

 Yohana 1 : 12 ( Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake )

BW KILINDU AKISOMA NENO KATIKA IBADA



 Yesu anafananisha Ufalme wa Mungu na
-    Punje ya haradali
     Mathayo 13:31-32 ( Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake;
32 nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake. )


                 Maana yake ni hii mtu anapo okoka huonekana ni jambo dogo na la kawaida lakini anapo zidi kukua katika wokovu anafanyika mtu wa muhimu na wa kutegemewa katika jamii na taifa lake pia kwani anakuwa nuru ya ulimwengu akiangaza kwa matendo mema busara, hekima , maarifa , N.K.

Hitimisho kwa leo,  tumejifunza habari za Ufalme wa Mungu lakini pia upo ufalme wa shetani  ambao upo kinyume na Ufalme wa Mungu mfano katika Ufalme wa Mungu ukiambiwa useme kweli kwa shetani anasema useme uongo hivyo utajitambuaje kama upo katika Ufalme wa Mungu au shetani 

             Kama upo katika ufalme wa shetani haya yataonekana kwako ;-
Galatia5:19-21 (  19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.   )


             Kama upo katika Ufalme wa Mungu yataonekana kwako haya ;-
Galatia 5:22 -23 ( 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna 

 NB:    
      Nilazima mtu uwe katika ufalme mmoja kama haupo ka Mungu basi upo kwa shetani  AMUA SASA KUWA KATIKA UPANDE WA MUNGU ILI UFANIKIWE.

      Kama bado hujaokoka na unahitaji kuokoka tafuta sehemu tulia afu fuatisha sala hii ya toba

(          ( (Bwana Yesu nipo mbele zako mimi mwenye dhambi naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizo zifanya  futa jina langu katika kitabu cha hukumu na andika jina langu katika kitabu cha uzima ewe shetani ninakukataa na kazi zoko zote pia kuanzia sasa mimi ni mtoto wa MUNGU ninafuta maagano na mikataba yote nilioingia na wewe shetani katika jina la Yesu, EEEYesu nitumie kama upendavyo amina ) 

            Kama umesema sala hii kuanzia sasa umeokoka tafuta kanisa la walio okoka ili uweze kupata mafundisho ya msingi yatakayo kusaidia lakini pia kama upo Zanzbar karibu kanisani kwetu PAG Chukwani kanisa lipo karibu na kambi ya Jeshi , kama unakuja na daladala shuka Chukwani mwisho afu chukua bodaboda waambie wakupeleke kanisa la walokole au kwa Mchungaji Amosi

Mungu akubariki

MCHUNGAJI AMOSI LUKANULA KATIKA AKIFURAHI KATIKA UWEPO WA BWANA

Mawasiliano
Simu ya Mchungaji      0713 -254045
                                     0766- 119116
Simu Wazee wa Kanisa 
                                     0778 - 226540
                                     0652 - 943220 
   
Mwandishi Baraka    0717- 192319

0 comments:

Post a Comment