Sunday, July 3, 2016

LEO KATIKA IBADA JUMAPILI TAREHE 03 JUL 2016


LEO KATIKA IBADA JUMAPILI TAREHE 03 JUL 2016
SOMO - IMANI
MWL: CHUNGAJI AMOSI LUKANULA
MCHUNGAJI KIONGOZI KANISA LA PAG CHUKWANI ZANZIBAR AKIFUNGUA IBADA KWA MAOMBI YA NGUVU

K
Praise and Worship Team YA PAG Chukwani wakiimba wimbo wa kuabudu mwanzo wa ibada 

 SOMO : IMANI
Luka 17 : 5 -6     
            Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani.
6 Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii. 


Imani maana yake ni 
            kutegemea au kusadiki au kutumainia  au kutazamia jambo ambalo bado haujaliona.   Hivyo kwa imani  japo hatujamuona Mungu lakini tunasema MUNGU yupo kwa sababu tu tumesikia na kwa mioyo yetu tukaamini 

 Imani imegawanyika katika makundi matatu  ambayo ni 
             1.    Imani ya MUNGU ( Kiroho)
             2.   Imani ya Madhehebu
             3.   Imani ya asili ( Kibinadamu)
               
Chanzo cha Imani ni kusikia 
                    Warumi 10:17 ( Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo)
               
                     Chanzo cha imani yeyote ni kusikia haijalishi ni imani ya namna gani , iwe ni imani ya kweli ama ya uongo chanzo chake ni kusikia aidha Neno la kweli ama neno la uongo kutoka kwenye chanzo cha ukweli ama uongo. Hivyo maisha yetu  yanaathiriwa na yale tunayo yasikia kutoka vyanzo mbalimbali
     
                       Kwa leo tuishie hapa jumapili ijayo MUNGU akipenda tutaendelea na somo letu hili juu ya Imani tutaanza kuichambua imani ya Kimungu .   Barikiwa 





BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO KATIKA IBADA YA LEO

MCHUNGAJI AMOSI LUKANULA AKIFAFANUA JAMBO KATIKA IBADA

MWIMAJI WA NJIMBO ZA INJILI CHARLES DANIEL AKIFANYA MAMBO YAKE
CHARLES DANIEL AKISEMA SHALOOM UBARIKIWE NDIO JINA KA WIMBO NA ALBAM ANAYOTARAJIA KUIZINDUA MWEZI WA TISA MWAKA 2016 AUDIO NA VIDEO NDANI YA ZANZIBAR
WAKATI WA SIFA MAMBO YALIKUWA MOTOMOTO
MCHUNGAJI KIONGOZI AMOSI LUKANULA AKIOMBA MAOMBI YA IMANI KWA AJILI YA KILA ALIYEFIKA KATIKA IBADA  

0 comments:

Post a Comment