Sunday, May 1, 2016

MAISHA YA WOKOVU NDIO KUOKOKA.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Wokovu ni nini?
Wokovu ni mpango Wa MUNGU kumuokoa mwanadamu kutoka dhambini, kutoka Katika mambo ya kidunia na kutoka katika hila za shetani.
Kuishi maisha ya wokovu ndio kuokoka kwenyewe.
Isaya 51:6 '' Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na haki yangu haitatanguka.''
Wokovu wa MUNGU ni kwa wateule na Wokovu wa MUNGU ni wa milele.
Watu wengine hudhani wokovu na kuokoka ni mambo mawili tofauti.
Kuna watu pia husema wao wanaishi maisha ya wokovu lakini ukiwauliza kama wameokoka watakuambia hawajaokoka, sijui watu hao wanakwama wapi.
Huwezi kumpokea YESU kisha unaishi maisha matakatifu harafu ukawa bado hujajua tu kama hayo maisha unayoishi ni maisha ya Wokovu na kwa sababu unaishi maisha ya wokovu yaliyo sahihi hakika wewe umeokoka.
Maisha ya wokovu ni maisha ya ushindi dhidi ya dhambi.
Anayeokoa ni mmoja tu ambaye ni BWANA YESU.
Ndio maana Biblia inamwita BWANA YESU jina lake jingine ni WOKOVU WETU.
BWANA YESU anaitwa Wokovu wetu.
Zaburi :27:1 ''BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?''
Faida ya kwanza ya mtu kuishi maisha ya wokovu siku zake zote ni uzima wa milele.
Faida nyingine ni ulinzi wa kipekee wa MUNGU.
Wokovu ni wa milele.
Mtu anayeishi maisha ya wokovu anatakiwa kuishi katika maisha hayo ya wokovu miaka yake yote.
Waefeso 6:17 ''Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la MUNGU;''
Maisha ya wokovu ni maisha matakatifu yanayomtii MUNGU na Neno blake.
Maisha ya wokovu humtii BWANA YESU na injili yake.
Maisha ya wokovu humtii ROHO MTAKATIFU na kila jambo lake.
Matendo 4:12 '' Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.''
Ukitaka kujipima kama unaishi maisha ya wokovu yaliyo sahihi basi angalia matendo yako kama ni matakatifu.
Jambo la pili angalia je unaishi kwa kutii Neno la MUNGU au maneno ya watu.
Jambo la tatu je ROHO MTAKATIFU ana sehemu gani katika maisha yako?
Kumbuka mwanadamu hawezi kuishi maisha sahihi ya wokovu kama mwanadamu huyo hana ROHO MTAKATIFU.
Biblia inahimiza jambo hilo ikisema;
''Tukiishi kwa ROHO, na tuenende kwa ROHO.-Wagalatia 5:25''
Wokovu ni muhimu Sana Kwa watu wote.
Wokovu uko pekee katika BWANA YESU.
Wokovu umekamilika.
Wokovu hujilinda wenyewe.
Wokovu hauhitaji nyongeza maana umekamilika.
Ndugu zangu, ni vizuri sana kila mmoja wetu akaishi maisha matakatifu ya wokovu.

Aliko BWANA YESU ndiko huko wokovu iliko.
Kama huna BWANA YESU Moyoni mwako hakika huna wokovu.
Kama huna Wokovu wa KRISTO hakika huna uzima wa milele.
Aliko BWANA YESU ndiko huko uliko na wokovu wake.
Luka 19:9 ''YESU akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu.''
BWANA YESU huambatana na wokovu wake. Tukimpokea BWANA YESU tumeupokea na wokovu wake.
Tukiishi maisha matakatifu ya wokovu hakika BWANA YESU yuko upande wetu.

Kwa Tuliookoka na Tunaoishi maisha matakatifu duniani.
-Makao yetu yako mbinguni, ni makao yasiyoharibika

Mathayo 6:19-21 ''Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako. ''
-Wateule wa KRISTO tutakuwa wa milele.
-Mbingu ni ya milele.
-Vitu vya mbinguni ni vya milele.
-Furaha ya milele
-Na uzima wa milele

1 Petro 5:4 ''Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.''
Kumpokea YESU leo kwa wewe ambaye hujaokoka ni jambo muhimu zaidi kwako.
Kuishi maisha matakatifu siku zote ni hazina yako ya milele.
-Waliookoka tuna baraka ya milele

1 Petro 1:4 '' tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu.''
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

0 comments:

Post a Comment